Picha ya madjoz - Page 3







Kama faili limebadilishwa kutoka hali yake ya awali, inawezekana kwamba vipengele kadhaa vitakuwa tofauti kuliko hali ya picha ilivyo sasa.
Katika ngoma hii ya ‘I Like It’ amemshirikisha Sho Madjozi ambaye amejijengea umaarufu mkubw kwa kuitangaza lugha ahimu ya Kiswahili.
Madjozi ndiyo huyu aliimba wimbo wa John Cena ambao ulisababisha AGOSTI 17, mwaka jana, mcheza myeleka, rapa, actor, comedian huyo wa Marekani, John Cena, kuifanya Afrika Kusini ilipuke kwa shangwe.
Cena alipost Instagram, cover ya jarida la "Successful Woman" yenye kumwonesha mrembo talented, mwandishi, mtangazaji na mwanamuziki wa Afrika Kusini, Sho Madjozi.
Kwa wafuatiliaji wa akaunti ya Cena Instagram, huwa ana upuuzi mwingi. Hupost picha bila kuweka maelezo yoyote. Ujumbe wake wote huumaliza kwenye picha.
Cena katika upuuzi wake, huchukua picha ya staa wa Hollwood na mcheza myeleka mstaafu, Steve Austin ‘Stone Cold’ na kuichezesha na picha za wengine, kwamba Stone Cold yumo ndani ya mastaa wengine.
Agosti 30, mwaka jana, Cena akapost picha ya Sho Madjozi tena lakini akaiwekea mikono ya Stone Cold. Picha ikasomeka "Stone Cold Sho Madjozi". Afrika Kusini na Afrika ikalipuka tena. Cena ni huge-man duniani. Kumpost Sho Madjozi ni bonge la endorsment.
Unajua kwa nini? Sho Madjozi ana wimbo unaitwa "John Cena", halafu ngoma yenyewe ni ya Kiswahili.
Novemba 8, mwaka jana, Sho Madjozi alipata bahati ya kualikwa kwenye shoo ya televisheni ya mwanamuziki supastaa wa Marekani na duniani, Kelly Clarkson. Inaitwa Kelly Clarkson Show.
Kelly na Cena wakamsapraiz Sho Madjozi. Akiwa anapaform wimbo "John Cena", mara Cena mwenyewe akaingia na kucheza. "Unajifanya hunioni labda mi ni John Cena, uliniona mfungwa wako labda mi ni Madiba. Unajifanya mwalimu wangu labda we ni Nyerere". Madjozi alipomuona Cena si akapata uchizi?



















